Saturday, April 13, 2013

HUU NDO UFISADI MKUBWA WA JOHN CHEYO CHINI YA "KOFIA YA BUNGE"

 John Momose Cheyo mwanasiasa wa siku nyingi ametumia cheo chake cha Uenyekiti wa Kamati ya PAC, kujinufaisha kupitia kampuni ya mdogo wake anayejulikana kwa jina la Sylvester Maghembe Cheyo ambaye anamiliki kampuni inayoitwa ATLAS PLUMBERS AND BUILDERS LTD.

Kwa kipindi ambacho Mheshimiwa Cheyo amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya Bunge kampuni ya ATLAS Plumbers amd Builders imepata miradi ifuatayo katika mashirika ya Serikali ambayo yapo chini ya Kamati iliyokuwa inaoongozwa na Bwana Mapesa.

1. TCRA - Headquarters DSM Sam Nujoma Road - Fire fighting installation and Plumbing 2010

2. LAPF - Millenium Towers - Phase Two DSM - Fire Fighting Installation 840,000,000/= Mwaka 2011- Bado mradi unaendelea

3. PPF Projects at UDOM
(i) Administration Block - Plumbing and Fire Fighting Installation 526,780,000/= Mwaka 2011
(ii) Dispensary Block - Plumbing and Fire Fighting 340,450,000/= Mwaka 2011
(iii) Library Block - Plumbing and Firefighting 613,584,000/= Mwaka 2011

4. BOT - Safe Custody Dodoma - Fire Fighting and Plumbing installation 687,504,800/= Mwaka 2011 bado unaendelea

5. LAPF Dodoma
- Fire fighting Installation 780,000,520/= March 2012 - Unaendelea
- Plumbing system 810,250,451/= March 2012 - Unaendelea

6. National Audit
- Dodoma Fire fighting and Plumbing system Installation 1,160,980,120/= Billion Moja na Million mia moja na Sitini.......... April 2012

7. EAC Headquarters - Fire Fighting and Plumbing 790,420,070/= 2011 Unaendelea

Makampuni ya Plumbing yapo mengi na yenye uwezo wa kutosha lakini kazi zote hizi ilipewa ATLAS Plumbers na ufanyaji wa kazi sio wa kuridhisha maana Consultant wa miradi hiyo hapo juu ambao ni MD kwa miradi ya PPF, CSC kwa miradi ya LAPF hawaridhishwi na Utendaji wa ATLAS lakini wamekuwa hawana sauti sababu ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge. Na ndio sababu huwezi kumsikia Mh. Mapesa akihoji namna mashirika hayo yanavyotumia pesa ya umma.

No comments: