Saturday, April 13, 2013

NYARAKA NZITO ZA CCM ZAVUJA...

Taarifa za ndani kabisa zilizopatikana kutoka kwa Waandishi wa habari,Vyombo vya usalama na ndani ya CCM kwenyewe zinaonyesha sakata la Kuteswa kwa Kibanda na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi Mkurugenzi wa usalama wa Chadema ndugu Alfred Lwakatare linachukua sura mpya na mapya yamefichuka kwa ushahidi.

Dennis Msacky ambaye ni mhariri wa Mwananchi aliyehusishwa na kuwa mojawapo wa watu waliopangwa kutekwa,amekua akifanya mawasiliano na Ludovick Joseph Lwezaura kama ifuatavyo

Tarehe 27/12/2012: Dennis Msacky kupitia simu ya mkononi namba 07643310**  aliwasiliana kwa simu na Ludovick Joseph kupitia simu namba 07539271**  akiwa Tamal hotel,Mwenge jijini dar-Es Salaam. Hii ilikua siku moja kabla ya mkanda wa video uliowekwa youtube kurekodiwa.mkanda ulionyesha kuwa ulirekodiwa kesho yake yaani tarehe 28/12/2013
Tarehe 30/12/2012 Dennis Msacky kupitia simu namba 07643310**  aliwasiliana na Ludovick kupitia simu namba 07539271** mnamo saa tano na dakika 8 asubuhi akiwa Iringa. Hii ilikua siku moja baaada ya Mwigulu Nchemba kutangaza kupitia kituo cha televisheni cha Star TV kwamba anao mkanda unaoonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji..

 Tarehe 31/12/2012 Dennis Msacky alimpigia simu ludovick kwa namba hizo hizo mnamo saa moja kamili usiku (19:00),wakati huo Ludovick akiwa Tegeta Huyu ni mtu aliyepangwa kutekwa,lakini alikua na mawasiliano na kijana Ludovick ambaye ni Mtuhumiwa.

Pandikizi Ludovick alikua na mawasiliano na Mwigulu nchemba na pia zimepatikana envidence za kutumiana fedha na mwigulu Nchemba alikiri hilo.

Duru mpya zimeendelea kuonyesha kuwa Dennis Msacky anatumika kwa kiwango cha kutisha katika kuihujumu CHADEMA akishirikiana na Rafiki yake ambaye ni waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi,Mwigulu Nchemba,Nape Nnauye,Zitto kabwe na Steven Wassira.

Lengo la mipango hii ni kutaka:
Mosi,Chadema kichukiwe na waandishi wa habari.

Pili,Kutaka Chadema kionekane chama cha kigaidi ili kifutwe .

Tatu,Zitto alipoandika barua kwa katibu mkuu wa chadema haikua bahati mbaya.na hata ilipovujishwa  na yeye mwenyewe ilikua ni mkakati wa Zitto kujionyesha kwamba yeye ni rafiki zaidi wa waandishi wa habari na msimamo wake baada ya kuona unakwama akaamua kujitoa.

Zitto anajua mkakati wote kuanzia mwanzo hadi mwisho.Barua yake aliiandika kwa makusudi na alijua ataivujisha baada ya kikao cha kamati kuu akishirikiana na Msafiri Mtemelwa siku ya ijumaa iliyopita tarehe 5/04/2013 na kisha kukaa kimya hadi siku iliyofuata siku ya jumamosi tarehe 06/04/2013 alipojitokeza na kutoa tamko la kuthibitisha barua hiyo imevuja na kujaribu kuihusisha ofisi ya katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa Chadema pamoja na kuongea mambo ambayo yeye sio msemaji wa vikao vya kamati kuu kinyume na kanuni,miongozo na taratibu za chama hicho ..

Ikumbukwe kuwa Gazeti la Mwanahalisi lilichapisha mawasiliano ya Zitto na Dennis Msacky wakipanga kukihujumu Chadema miaka iliyopita.kitendo
hicho kilichafua sifa ya Dennis Msacky na chombo anachofanyia kazi.

Hadi muda huu duru za ndani kutoka mwananchi Communications ltd zinadai kuwa uongozi na hata wafanyakazi wa chombo hicho hawakufurahishwa na uhusika wa dennis Msacky katika kuhujumu vyama vya upinzani akishirikiana na vyombo vya dola huku wakihisi kuwa amehusika kwa namna moja ama nyingine na matukio mabaya ya kisiasa yaliyotokea likiwepo hili la Kibanda,la Dr.Ulimboka n.k

No comments: