Monday, July 16, 2012

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AWATAKAWANANCHI KUJITOKEZA KATIKA SENSA ILI WACHANGIE MAENDELEO

MKUU wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanajitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi la Sensa kwani sensa ndio chanzo cha Serikali kusaidia jamii
Mulongo aliyasema hayo jijini Arusha leo wakati akifungua mafunzo kwa wakufunzi zaidi ya 100 wazoezi hilo la Sensa  ambalo lintarajiwa kuanza hivi karibuni

Mkuu huyo alisema kuwa kila mwananchi wa mkoa wa Arusha anapaswa kujua na kutambua kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo yake na hivyo kamwe wasikubali kupotoshwa na baadhi ya watu

Alisema kuwa mpaka sasa ndani  ya mkoa wa arusha hakuna tetesi zozote ambazo zimejitokeza na kuwasihi watu wasiweze kushiriki katika zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kufanyika hivi katibuni

Mbali na hayo aliwataka wadau wa zoezi hilo ambao ni Wakufunzi kuhakikisha kuwa wanatumia uzoefu wa kisasa katika zoezi hilo ili waweze kufikia malengo mbalimbali ambayo yanakusudiwa katika zoezi la Sensa kwa mwaka huu

Alifafanua kuwa zoezi hilo lina umuhimu mkubwa sana na kwa hali hiyo ni vema kama watendaji wakuu wakawa makini kwa kuhakikisha kuwa wanakabiliana na Vikwazo ambavyo vinaweza kutokea wakati  wa zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi linaloanza hivi karibuni.

“kama zoezi hili litakwama ni hasara kubwa sana kwa Serikali na hata kwa maendeleo ya jamii sasa nawasihi sana ninyi wadau hakikisheni kuwa mnakuwa makini na kama mdau hanaona kuwa atakuwa moja ya kikwazo cha Sensa ni bora akasema mapema na ajitoe kuliko kuwa chanzo cha kushindwa kufikia malengo”aliongeza Bw Mulongo

Chanzo Fullshangwe - Arusha

No comments: